Vipimo
Unga 1 Kikombe cha chai
Iliki ya unga ½ Kijiko cha chai
Chumvi ½ Kijiko cha chai
Mayai 2
Mafuta ¼ Kikombe cha chai
Sukari ½ Kikombe cha chai
Sukari ya hudhurungi
(brown sugar) ⅓ Kikombe cha chai
Mtindi (yogurt) ⅓ Kikombe cha chai
1. Washa oveni moto wa 350°F.
2. Paka mafuta chombo utakayopikia keki, kisha nyunyiza unga na gonga iliyozidi.
3. Kwenye bakuli la kiasi, changanya pamoja unga, baking soda, iliki, na chumvi weka kando.
4. Katika bakuli nyengine, piga mayai, sukari, mtindi, na mafuta mpaka ilainike.
5. Polepole changanya mchanganyiko wa mayai kwenye wa unga hadi ilainike; kisha tia karoti.
6. Mimina kwenye chombo uliyo tayarisha na uvumbike kwa dakika 40 - 45.
7. Kisha iache ipoe kwenye sufuria dakika 15 halafu pindua na iache ipoe kabisa.
Post a Comment