Featured

    Featured

MAPISHI: Keki Ya Karoti

Vipimo

Unga                                           1 Kikombe cha chai
Baking soda                                 1 Kijiko cha chai
Iliki ya unga                                ½ Kijiko cha chai
Chumvi                                        ½ Kijiko cha chai
Mayai                                           2
Mafuta                                               ¼ Kikombe cha chai
Sukari                                          ½ Kikombe cha chai
Sukari ya hudhurungi
(brown sugar)                               Kikombe cha chai
         
Mtindi (yogurt)                             Kikombe cha chai
Karoti iliyokaruzwa                     1 Kikombe cha chai (kama karoti 2)
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
 
1.    Washa oveni moto wa 350°F.

2.    Paka mafuta chombo utakayopikia keki, kisha nyunyiza unga na gonga iliyozidi.

3.    Kwenye bakuli la kiasi, changanya pamoja unga, baking soda, iliki, na chumvi weka kando.

4.      Katika bakuli nyengine, piga mayai, sukari, mtindi, na mafuta mpaka ilainike.
5.    Polepole changanya mchanganyiko wa mayai kwenye wa unga hadi ilainike; kisha tia karoti.

6.    Mimina kwenye chombo uliyo tayarisha na uvumbike kwa dakika 40 - 45.

7.    Kisha iache ipoe kwenye sufuria dakika 15 halafu pindua na iache ipoe kabisa.

8.    Tengeneza sukari laini (icing sugar) ½ kikombe na vijiko 2 vya maji na unyunyizie juu; na ikisha kauka itakuwa tayari kuliwa.

PUNGUZA UNENE KWA ASALI NA LIMAU

Unene wa mwili wa kupita kiasi
(obesity) ni miongoni mwa matatizo
ya kiafya yanayowasumbua watu
wengi. Kuna njia nyingi za kufanya ili
kupunguza unene, yakiwemo mazoezi
ya viungo na kutumia baadhi ya
vyakula kimpangilio.

Unene wa kupita kiasi ni hali
inayomtokea mtu pale mafuta
yanaporundikana kwenye ‘tishu’ za
mwili hivyo kusababisha matatizo
kwenye moyo, figo, ini, viungio vya
mwili kama vile magoti, n.k.

Halikadhalika, watu wenye matatizo
ya uzito wa kupindukia huweza
kupatwa na matatizo pia ya shinikizo
la damu, kisukari, magonjwa ya msuli,
ini na hata kibofu cha mkojo. Kwa
ujumla unene siyo mzuri na ni chanzo
cha maradhi mengi hatari. Kama
unajali afya yako, unene ni wa
kuogopwa kama ukoma.

Habari njema kuhusu tatizo hilo ni
kwamba unaweza kujikinga nalo kwa
kutumia asali na kama tayari unalo
unaweza kulitibu au kulidhibiti kwa
kutumia asali kwa kuchanganya na
limau kwa utaratibu maalum.

Asali ni tiba nzuri ya kiasili ya kutibu
tatizo la unene pamoja na shinikizo la
damu, kwani hupunguza mafuta
mabaya mwilini (bad cholesterol) kwa
kuyageuza mafuta ya ziada kuwa
nishati ya mwili. Mtu unaweza
kufunga kula vitu vingine na badala
yake ukatumia asali na limau tu kama
tiba ya unene, bila kupoteza hamu
yako ya kula au nguvu ya mwili.

JINSI YA KUTENGENEZA ASALI NA
LIMAU

Kuna imani potofu kwa baadhi ya
watu kuhusu limau na asali kuwa ni
sumu. Ukweli ni kwamba
mchanganyiko huu ambao ni wa
‘alkalaini’ mwilini siyo sumu bali ni
tiba kwa matatizo mengi ya kiafya,
likiwemo tatizo la unene.

Ili kupata mchanganyiko sahihi, weka
asali mbichi kwenye kijiko kimoja
kidogo kwenye glasi yenye maji ya
uvugu uvugu (siyo yaliyochemka),
kisha weka vijiko viwili vya juisi ya
limau (saizi ya kijiko cha chai) halafu
koroga na unywe mchanganyiko huo.

Kunywa mchangayiko huo asubuhi
kabla hujala kitu chochote au
unaweza kunywa mchangayiko huo
kila baada ya mlo mkubwa au ulaji wa
vyakula vyenye mafuta mengi,
mchanganyiko huo husaidia usagaji
wa chakula na uondoaji wa sumu
mwilini.

Katika kutekeleza mpango huu kwa
lengo la kupunguza unene, usisahau
kuzingatia suala la ulaji wa vyakula
vyenye faida mwilini na
vinavyoruhusiwa kiafya. Itakuwa ni
kazi bure iwapo utatumia tiba ya asali
huku ukiendelea na ulaji wa vyakula
usiyokubalika kiafya. Halikadhalika
mazoezi ya mara kwa mara ni suala
muhimu kuzingatiwa.

COCKTAIL YA MATUNDA NA ASALI
Aidha, katika kuimarisha kinga na
kuondoa sumu zaidi mwilini, unaweza
kutengeneza mchangayiko wa
matunda mengi (fruit cocktail) pamoja
na asali na kisha ukanywa. Kufanikisha
hilo, chukua matunda kama vile epo,
nanasi, zabibu, machungwa, karoti na
mapera, yaandae vizuri kisha weka
kwenye blenda na tengeneza juisi,
bila kusahahu kuweka vijiko viwili vya
asali mbichi. Tengeneza kiasi cha glasi
moja na kunywa wakati ule ule kwa
lengo la kupata vitamini zote bila
kupotea.

Mwisho, ili kujiepusha na unene wa
kupindukia, usipende kula kupita kiasi,
hasa vyakula vyenye mafuta, ili hali
hufanyi mazoezi wala hufanyi kazi
yoyote ya shuruba. Unene ni dalili ya
maradhi, jiepushe nao.

www.CodeNirvana.in

Translate

Total Pageviews

Copyright © Umm Fashion | Designed By Balozi wa mtaa